The House of Favourite Newspapers

NDOA YA CHAZ YAPIGWA ZENGWE

UMBEYA ni suna na pia unaongeza vitamini mwilini! Siku moja baada ya kufungwa, ndoa ya mwanamuziki mahiri wa muziki wa Dansi Bongo, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ ambaye kwa sasa anaitumikia Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, imepigwa zengwe matata, Risasi Jumamosi lina ubuyu kamili.

 

Taarifa zilizolifia gazeti hili zilidai kuwa mwanamke ambaye Chaz Baba alimuoa Alhamisi iliyopita, Mariam Chavala aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa mkubwa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.

 

Kwa mujibu wa chanzo makini, mwanamke huyo mpaka sasa ana ukaribu na familia ya Kiba baada ya kujitoa vilivyo kwenye harusi ya mdogo wa Kiba, Zabibu Kiba wakati anaolewa na Abdi Banda hivyo watu wanaowafahamu wamekuwa wakizua minong’ono.

 

“Mpaka leo Mariam anakubalika kwenye familia ya Kiba na ndiye aliyeaminika angeolewa na jamaa huyo,” kilidai chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa familia ya Kiba. Baada ya kupewa ubuyu huo wa motomoto, Risasi Jumamosi lilimtafuta Mariam ambapo mambo yalikuwa hivi;

MSIKIE MARIAM

Risasi Jumamosi: Hivi karibuni umebadilisha jina kwenye mtandao wako wa kijamii na kujiita mke halali wa Chaz Baba, hilo unalizungumziaje?

Mariam: Kubadilisha jina sioni kama ni tatizo hata kidogo maana nimeamua tu kujiita hivyo.

Risasi Jumamosi: Lakini inasemekana wewe ndiye mkewe mtarajiwa?

Mariam: Mimi sina cha kuzungumza, uzuri harusi haifichwi, utajua kila kitu.

Risasi Jumamosi: Mbona huko nyuma inadaiwa ulikuwa ni mchumba kabisa wa halali wa Kiba hadi kwao ulikuwa unakubalika sana, ilikuwaje?

Mariam: Kiba simfahamu mimi…ndiyo nani kwanza? Yaani kwa mara ya kwanza ndiyo ninalisikia jina lake kutoka kwako.

Risasi Jumamosi: Kwa hiyo wewe siyo mke mtarajiwa wa Chaz Baba?

Mariam: Ni vizuri zaidi hata maswali akaulizwa Chaz Baba. Kwa maana mimi mwenyewe sipendi

maisha yangu yawe wazi hata siku moja. Baada ya kuzungumza na Mariam, Risasi Jumamosi lilimtafuta Chaz Baba ambaye alikataa katakata kumzungumzia mkewe huyo akisema mwanamke huyo hapendi kabisa mambo yake yawe wazi. “Unajua bora mniandike mimi, lakini siyo mke wangu maana haya mambo hayapendi kabisa,” alisema Chaz Baba.

 

Hata hivyo, pamoja na kwamba Mariam anakanusha kufahamiana na Kiba, lakini kuna baadhi ya picha zake kwenye ukurasa wake wa Instagram akionekana akiwa na ndugu wa Kiba kama Zabibu na Abdu Kiba. Habari ya uhusiano wa Kiba na Mariam uliwahi kuandikwa na gazeti mojawapo la Kampuni ya Global Publishers, enzi hizo kabla ya jamaa huyo kumuoa mrembo kutoka jijini Mombasa nchini Kenya, Aminah Khaleef.

Comments are closed.