visa

NELLY AYASIKITIKIA MAISHA YA UJANA

Mwanamitindo na mrembo ambaye ameshika mataji mbalimbali Bongo likiwemo la Miss Universe Tanzania 2011,amefunguka hakuna kitu anachosikitikia kama ujana ambao warembo mbalimbali wanapitia.  Akipiga stori mbili tatu na Za Motomoto, Nelly alisema kuwa, unapokuwa upo juu na ni kijana kuna vitu vingi ambavyo usipokuwa makini unajikuta unaingia katika mambo ambayo hayafai na ni kinyume kabisa hata kwa jamii nzima maana hapo ndipo pa kujifunza na kutengeneza mambo mema na mazuri.

“Mtu asikwambie kitu jamani ujana ni mbaya sana, maana usipokuwa makini na muangalifu lazima utandumbukia shimoni kwani ndio kipindi cha kufanya mambo mengi ambayo unakuta hata nyumbani kwenu hawayapendi na hata jamii haipendezwi nayo na mwisho wa siku unapotea katika ramani,” alisema Nelly.
Toa comment