The House of Favourite Newspapers

NUH MZIWANDA: Kuoa Tena Namuachia Mungu

0

 

NUH MZIWANDA: Kuoa Tena
Nuh Mziwanda.

NUH MZIWANDA: Kuoa Tena…

MWANAMUZIKI Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ ambaye hivi karibuni mkewe, Nawal alifunga ndoa na mwanaume mwingine amefunguka kuwa, kwake kuoa tena anamuachia Mungu.

Akibonga na Mikito Nusunusu, Nuh alisema baada ya mkewe kuondoka na kuamua kuolewa bila kumpa talaka suala la kuoa au kutokuoa anamuachia Mungu na kwamba hajaathirika chochote kuhusiana na mkewe kumuacha ila anachofanya kwa sasa ni kuongeza bidii katika kazi.

“Namwachia Mungu ndiye anayejua kama nitaoa au sitaoa tena, ikitokea sawa na isipotokea inakuwa sawa tu kwa sasa moyo wangu una amani tele na nimerudi kwenye dini yangu ya Kikristo, kuhusu mwanangu ataendelea kuwa wangu na mahitaji yote muhimu natoa kama baba,” alisema Nuh.

 

STORI: GLADNESS MALLYA

 

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Shamrashamra Mapokezi ya Watoto wa Shule ya Lucky Vincent KIA

Leave A Reply