The House of Favourite Newspapers

Obrey Chirwa Asaini Azam, Walitangaza ‘Kumtema’


Mshambuliaji Obrey Chirwa, ataendelea kuitumikia Azam FC na tayari leo mchana amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja.

Chirwa raia wa Zambia alikuwa ni miongoni mwa wachezaji tisa waliotangazwa kuachana na klabu hiyo Jumanne iliyopita lakini taarifa rasmi iliyotolewa leo na uongozi wa timu hiyo imeeleza kuwa pande zote mbili zimeshafikia makubaliano.

Taarifa hiyo imesema Chirwa ameanza maandalizi ya msimu mpya na kikosi cha timu hiyo jana.

Comments are closed.