ODEMBA ATESWA NA K LYNN

Miriam Odemba

MWANAMITINDO aliyewahi kujizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, Miriam Odemba amesema aliumizwa sana na kushindwa kukaa muda mrefu Bongo kumfariji rafiki yake Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K Lynn’ maarufu kama Jack Mengi, baada ya kufiwa na mumewe Dk. Reginald Mengi, ambaye amezikwa jana, Machame, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.  Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa njia ya simu, Odemba alisema, alitamani sana kuwepo kipindi chote na kumfariji rafiki yake huyo, lakini majukumu mengine ya kazi yalimtinga.

“Kwa kweli naumia sana, nilitamani mno kuwa karibu sana na rafiki yangu lakini kazi imenifanya nirudi Paris (Ufaransa), ndio maana kuna kipindi natamani sana kurejea nyumbani na kuendeleza majukumu yangu ya kila siku, ila Jack ameniumiza sana kwa kweli. Namuomba awe na moyo wa imani, Mungu atasimama naye katika hili,” alisema odemba


Loading...

Toa comment