×

Pasta Azindua Nguo za Ndani Zenye Sura Yake Kuwasaidia Warembo Kupata Waume

Pasta  Dr J.S. Yusuf wa  wa Kanisa la Touch for Recovery Outreach International mjini Abuja  amezindua nguo za ndani na sindiria zenye chapa ya picha yake ili kuwasaidia wanawake waseja wanaotamani kuolewa kuwavizia waume zao.

 

Kwa mujibu wa pasta Dr J.S. Yusuf, aliagizwa na Mungu kuzindua chupi hizo za ‘baraka’ ili kufungua milango ya ndoa Mwaka Mpya.

 

Mchungaji huyo alinukuu mstari kwenye kitabu cha Hesabu 23:20 unaosema“Tazama nimepokea amri ya kubariki, naye amebariki, wala siwezi kubadili.”

 

Chupi hizo zinasemekana pia kuwasaidia wanawake kujikinga na magonjwa na kupata bahati njema wakiwa na wanaume.

 

Leave a Comment