The House of Favourite Newspapers

Penzi la Zuchu na Diamond Balaa, Wazazi Kimeumana

0

Baada ya tetesi kusambaa katika mitandao ya Kijamii juu ya mahusino ya Dimaond Platnumz pamoja na mrembo Zuchu, sasa Inasemekana kwamba Mama Dangote na Khadija Kopa hawapiki chungu kimoja tena.

 

Taarifa zinadai kwamba Mama mzazi wa Diamond, Mama Dangote ameshindwa kuamini kilichotokea kwa mtoto wake kwenda kumpenda Zuchu. Unaambiwa huko Diamond Platnumz hasikii wala haambiliki Mama yake amepiga kelele yanapitia sikio la upande wa kulia yanatokea sikio la upande wa kushoto, achana na kitu mapenzi kabisa.

 

Chanzo chetu kimedai kwamba Mama Dangote imefika sehemu ameanza kusema kwamba upendo wa Diamond kwa Zuchu siyo wa bure kuna Jambo mtoto wake huyo amefanyiwa na Bi Kopa ili, Mond, Simba chibu Dangote ampende Zuchu. Hadi hapo kimeumana kipande hicho unaambiwa hawapiki chuku kimoja tena wazazi hao wawili.

 

Mama Dangote inadiwa kwamba amesema kwamba ndoa haiwezi kufungwa kwani yeye anachokiona mwanae siyo wa kumuoa Zuchu na hataki kusikia kabisa neno ndoa. Mnyapiaji ameendelea kudai kwamba katika kudhihirisha hilo ndio maana hakuna hata interview moja aliyoonekana anaongelea penzi la Mtoto wake na Zuchu.

 

Lakini kwa upande wa pili yaani Bi Khadija Kopa ambaye ni Mama Zuchu yeye amesema kwamba ikitokea Diamond Platnumz akaamua kumuoa mtoto wake yeye hana pingamizi lolote yaani yupo tayari hata kesho ndoa ifungwe, Jamani patamu hapo wakati huo upande wa pili ndoa haitakiwi kabisa na wala hawataki kuiisikia.

 

Diamond na Zuchu wao wamegoma kabisa kuongea lolote kuhusu penzi hilo, zaidi kabisa Diamond yeye ndio hataki kusikia mtangazaji yoyote akimuhoji kuhusu Zuchu. Kwani inadaiwa kwamba anaona aibu kwa kula kifaranga chake kutoka Wasafi. Zuchu na yeye anasema kwamba Diamond ni kaka yake kwenye muziki na boss wake pia.

Leave A Reply