The House of Favourite Newspapers

Pichaz + Video: Mazishi ya Baba wa Amina Chifupa Leo Kisutu, Dar

1
Mwili wa marehemu mzee Chifupa ukipelekwa mahali pa kuzikiwa katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
Mwili ukiingizwa kaburini.
Shughuli ya kuzika ikiendelea.
Abdurahman, mjukuu wa mzee Chifupa, ambaye ni mtoto wa marehemu Amina Chifupa, akimlilia babu yake wakati wa mazishi.
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete (mwenye miwani) akiongea jambo la Abdulrahman wakati wa mazishi.

KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kapteni Hamisi Chifupa ambaye alikuwa baba wa  aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa (Vijana) wa chama hicho, Amina Chifupa leo alizikwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar.

Mzee Chifupa alikutwa na umauti Ijumaa iliyopita majira ya saa mbili usiku baada ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi uliopelekea kifo chake.

Mazishi ya kada huyo yalihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mbunge wa Chalinze (CCM) Ridhiwan Kikwete na  Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara) Philip Mangula.

Katika mazishi hayo mjukuu wa marehemu huyo Rahmanino Mpakanjia aliwatia simanzi waombolezaji kwa jinsi alivyokuwa akilia katika hatua mbalimbali za mazishi hayo hasa mwili huo ulipokuwa ukifukiwa.

(Picha/Habari: Richard Bukos/GPL)

1 Comment
  1. […] Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), marehemu Amina Chifupa, kumpoteza babu yake, mzee Hamis Chifupa aliyefariki dunia wiki chache zilizopita, ameelezea maisha yake kwa sasa baada ya kufariki kwa babu […]

Leave A Reply