The House of Favourite Newspapers

POGBA ANAKULA BATA DUBAI

BAADA ya msimu wa Ligi Kuu England kumalizika, staa wa Manchester United, Paul Pogba ameamua kwenda Dubai na mchumba wake, Maria Salaues na mtoto wao kula bata.

 

Wawili hao walitupia picha kwenye Mtandao wa Instagram wakiwa wanakula bata ikiwa ni sehemu ya mapumziko yao.

 

Pogba anayewindwa vikali na Real Madrid, bado hajaweka wazi mustakabali wake wa kuendelea kusalia United kwa msimu ujao. Kiungo huyo yupo tayari kuondoka United alipokaa kwa miaka mitatu na kutua Madrid, lakini Madrid inatajwa kwamba inaweza isitoe pauni milioni 160 kama ada ya uhamisho ya mchezaji huyo.

 

Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer, anataka kumbakisha Pobga kikosini kwake na tayari amemuahidi unahodha msimu ujao.

Comments are closed.