Poshy Queen Afunguka Safari Yake Ya Bunge, Dodoma

Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’ akiwa katika picha na wabunge kwenye Viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

SIKU chache baada ya picha zake kusambaa akionekana akirandaranda na wabunge tofauti kwenye Viwanja vya Bunge jijini Dodoma huku kukiwa na madai kuwa ameenda kudanga, mrembo anayetikisa na umbo matata katika mitandao ya kijamii, Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’ amevunja ukimya juu ya safari yake hiyo.

Katika picha hizo ambazo hata yeye ameziachia katika ukurasa wake wa Instagram, Poshy anaonekana akiwa na furaha ndani ya kisketi ambacho kimemchora umbo lake vilivyo akishikana mikono ya salamu na wabunge mbalimbali akiwemo Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Profesa Jay’.

 

Katika habari zilizoenea, Poshy alidaiwa kuwa alikwenda jijini humo kudanga baada ya kupata mualiko na mbunge mmoja ambaye ana uhusiano naye.

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Poshy alifungukia madai hayo kuwa anawashangaa sana watu wote wanaomjadili na kumsemea maneno mabaya na kuuliza kuwa kwenda yeye bungeni ni makosa? “Watu bwana!

 

Mbona watu wana matatizo sana, yaani mimi kwenda bungeni ni matatizo jamani au sistahili kwa sababu kule kila mtu anakaribishwa kama mgeni wakati mimi kuna jambo lilinipeleka kule na nimejifunza vingi,” alisema Poshy mwenye kiuno cha nyigu.

 

Akiendelea kuzungumza na Ijumaa, Poshy alisema kuwa, asingependa kabisa watu waendelee kumjadili kuhusu yeye kwenda bungeni kwa sababu kila mtu anaruhusiwa kwenda, lakini alivyokwenda yeye ilikuwa kwa sababu maalum ya kipindi cha Bunge la Bajeti ambapo amesomea mambo ya usimamizi wa fedha katika Chuo cha IFM jijini Dar.

 

“Jamani watu wawe wanafikiri mara mbili hata mimi ni mtu na nina wazazi, vitu vingine wanavyovizungumza waangalie siyo kuongea tu bila sababu za msingi “Kule nilikwenda na mimi kuwasilisha mawazo yangu katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti, licha ya kuhudhuria hata nilivyokutana na baadhi ya wabunge niliwaambia mawazo yangu na wamesema watayafikisha huko,” alimaliza kusema Poshy. Poshy ametokea kujizolea umaarufu mitandaoni kutokana na umbo lake matata la namba nane ambalo inasemekana kuwa amelipata ghafla au ni la kutengeneza.

WATU KAMA HAWA NI BALAA, KUWA NAO MAKINI..TANZANIA MPYA


Loading...

Toa comment