POSHY WALA HAJAVIMBA KICHWA

Sexy lady anayetingisha kunako mitandao ya kijamii kutokana na umbo lake matata la kiuno cha nyigu, Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’ amesema, yeye kuwa msichana mrembo na mwenye umbo zuri hata siku moja hakumfanyi kuvimba kichwa na kujisahau. Poshy ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, uzuri wake haumfanyi kubweteka eti kwa imani kuwa shepu na uzuri wake vitamuingizia kipato. “Wengi wanafikiri hivi nilivyo ndiyo kunanifanya ninakula na kufanya kila kitu au kunipa mahitaji yangu,

kumbe vitu kama hivyo kwangu havina umuhimu, naona ni kawaida tu kwani ndivyo Mungu alivyoniumba. Badala yake ninatumia akili nyingi sana kujaribu kila siku nifanye nini niingize kipato,” alisema Poshy


Loading...

Toa comment