The House of Favourite Newspapers

Producer Emma The Boy apata ajali mbaya

imma

Producer maarufu wa THT, Emmanuel Maungu ‘Emma The Boy’ amepata ajali mbaya ya gari hivi punde maeneo ya Kabuku karibu na Segera, Tanga wakati akitokea Dar es Salaam kuelekea nyumbani kwao, mkoani Tanga.

Imeelezwa kuwa, Emma ameumia zaidi maeneo ya kifuani na shingoni na kilichomsaidia asiumie zaidi,  alikuwa amefunga mkanda.

Akizungumza moja kwa moja na mwanahabari wetu, kaka wa Emma amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa, kwa sasa mdogo wake huyo amelazwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Tanga akipatiwa matibabu kutokana na maumivu na majeraha makubwa aliyoyapata.

“Ni kweli Emma amepata ajali mbaya sana wakati akitoka Dar kwenda nyumbani Tanga, ameumia kifua na shingo na maeneo mengine, gari alilokuwa akisafiria limeharibika vibaya sana, tumuombee kwa Mungu aweze kupona,” alisema.

Aidha haijaelezwa chanzo cha ajali hiyo ni nini.

Msanii mwingine kutoka THT, Hamadai amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Emma The Boy ametengeneza nyimbo karibu zote za msanii Barnaba na wasanii wengine wa THT.

Taarifa zaidi za tukio hilo tutazitoa kadiri tutakavyozipata.

Comments are closed.