Q CHILLA ‘AOTA’ KURUDIA ENZI

MWANAMUZIKI wa Kizazi Kipya, Abubakary Katwila ‘Q-Chillah’ amejitapa kurudi katika gemu la muziki kama ilivyokuwa mwanzoni mwa miaka ya 2000 alipokuwa akitamba na ngoma mbalimbali ikiwemo Si Ulinikataa ambayo ilidaiwa kuwa ni historia ya kweli ya maisha yake.  Akizungumza na Risasi Vibes, kwenye Klabu ya Forty Forty iliyopo Tabata-Bima Dar, Q-Chillah anayetikisa na Ngoma ya Tikisa aliyoiachia hivi karibuni alisema kuwa itamtasaidia kumrudisha enzi zile alipokuwa gumzo na ngoma zake mbalimbali ikiwemo Si ulinikataa, Kosa langu na nyinginezo.

“Ndugu mwandishi kuna hii Tikisa na ngoma zangu zingine ambazo ziko jikoni zikishakamilika nakukuhakikishia ni lazima zinirudishe kwenye enzi zangu. “Kuna kipindi nilipotezwa na vishawishi na kuingia kwenye mambo yasiyofaa ambayo yalitaka kuniangamiza lakini sasa nimeshajitambua na ninachodili nacho ni kupiga kazi kwa juhudi maarifa. “Kama nilikuwa juu kwa juhudi zangu siwezi kushindwa kurudi tena baada ya kukaa na kutafakari nilipokosea na kugundua makosa yangu.”


Loading...

Toa comment