The House of Favourite Newspapers

QUEEN DARLEEN ANASEMA AMEJITOA KWA MONDI NA ZARI

DADA wa Diamond Platnumz, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ amesema katika maisha yake kamwe hawezi kuingilia malumbano ya mdogo wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ au Mondi na mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ anapoona hawako sawa.

 

Akizungumza na Amani, Darleen alisema kuwa siku zote yeye si mchangiaji kwenye tofauti za Diamond na Zari kwa sababu anaamini anaweza kufanya hivyo halafu siku wakipatana, akajikuta akikosa pa kuiweka sura yake.

 

“Sina tabia kabisa ya kuingilia ugomvi wa kaka yangu na wazazi wenziye, siyo Zari tu hata wengineo kwa hiyo hata kama kuna malumbano yao huwa nakaa kimya, naamini watayamaliza wenyewe mimi ni mtazamaji tu siku zote,” alisema

Stori: Imelda Mtema, Dar

BREAKING: Sakata la Daktari Aliyesimamishwa Kazi, RAIS Atoa Tamko!

Comments are closed.