QUEEN DARLEEN, FIRST LADY WA WCB ASHIKWA MKONO NA DULLY SYKES
MIAKA 15 nyuma katika muziki wa Bongo Fleva kwa upande wa wanamuziki wa kike, alikuwepo Mwanahawa Abdul Juma ‘Queen Darleen’ akikimbiza. Enzi hizo ulikuwa humwambii kitu kwani kama kujulikana na mastaa tayari alishajijengea jina baada ya kufanya kolabo na Kiba kwenye Ngoma ya Wajua akaja Inspector Haroun kupitia Mtoto wa Geti Kali kisha Dully Sykes kwenye Ngoma ya Historia ya Kweli na Maneno Maneno ambayo ilimpatia Tuzo ya Wimbo Bora wa Ragga/Dancehall kupitia KTMA 2012.
Wakati Queen anatikisa kwenye muziki miaka hiyo, kulikuwa na kaka yake, Nasibu Abdul ambaye alikuwa akirandaranda maeneo ya kwao, Tandale jijini Dar. Leo hii atashinda vijiwe vya Kwa Mtogore, kesho Tandale- Yemen!
Maisha yanakwenda kasi sana! Leo hii Nasibu Abdul anajulikana zaidi kama Diamond Platnumz ni staa anayetambulika ndani na nje ya nchi kumpita Queen.
Diamond amebadilisha kwa kiasi kikubwa soko la muziki wa Bongo Fleva. Amethubutu kuanzisha lebo ya kuwasimamia wasanii na kuiita Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo lebo hiyo leo ina wasanii wakali wanaotikisa ndani na nje ya Bongo.
Kama ulikuwa hujui, Queen ni first lady katika lebo hiyo akiwa ameshafanya kazi nyingi tofauti zikiwemo za kuwashirikisha wasanii anaounda nao lebo hiyo kama vile, Kijuso akiwa na Rayvanny, Mbali akiwa na Harmonize, Nitakufilisi, Touch na Muhogo.
Over Ze Weekend inampa heshima Queen ya kusimama kwenye ukurasa huu katika exclusive interview ambapo anafunguka mengi ikiwemo ishu ya kudaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Over ze Weekend: Najua umeanza muziki muda mrefu sana, ni changamoto gani umekutana nazo kama mwanamuziki wa kike?
Queen: Sikupata changamoto kubwa sana kupenya kwenye muziki kwa sababu nilikuwa nashikwa mkono na kaka Dully na Tudo. Labda changamoto ya kutongozwa na maprodyuza tu, lakini si vinginevyo.
Over ze Wekeend: Kuhusiana na kutongozwa na maprodyuza, uliingia kwenye line?
Queen: Ilikuwa ngumu kwani kila aliyekuwa akinitongoza, lazima nimwambie Dully au mjomba wangu, Tudo anawafuata.
Over ze Weekend: Unasema kuwa waliokushika mkono mmojawapo ni Dully vipi kuhusu Kiba? Wengi walikuwa wakijua ni ndugu yako?
Over Ze Weekend: Yaani Kiba tuliimba naye wimbo mmoja tu kwa sababu wote tulikuwa chini ya Lebo ya G-Lover na si vinginevyo. Pia mara nyingi sipendi kumuongelea kwa sababu nikiongea huwa inakuwa tofauti kwa jamii.
Over ze Weekend: Mara nyingi kwenye mitandao ya kijamii umekuwa ukirushiwa vijembe mbalimbali kutokana na uvaaji wako, unalizungumziaje hilo?
Queen: Ndiyo mavazi yangu nimeyazoea siku zote maana hadi wengine wanasema mimi ni msagaji, lakini mimi kwenye mavazi siko kihivyo!
Over Ze Weekend: Kwani ulishawahi kukumbwa na skendo hiyo ya usagaji?
Queen: Sana tu na hadi sasa hivi ipo mpaka najiuliza ni nani niliyewahi kumsaga, basi ajitokeze hadharani akiri hilo nijue.
Over Ze Weekend: Kuna kipindi ulisema huwa hutongozwi kwa nini?
Queen: (Kicheko) Unajua kwa kweli hata nikijichunguza waliowahi kunivua nguo hawafiki hata watano ndiyo maana nilisema hivyo.
Over Ze Weekend: Watu wengi wanajua wewe huna mtoto, lakini pia walishangaa kuona unasema kuwa ni msichana mbichi, hii imekaaje?
Over Ze Weekend: Kweli mimi ni mama wa mtoto mmoja wa kiume, Rooney na kuhusu kuwa msichana mbichi huo ni utani tu!
Over Ze Wekeend: Mara nyingi umekuwa hupendi kabisa kuweka uhusiano wako wa kimapenzi hadharani ni kwa nini?
Queen: Ni kwa sababu niliyenaye tuna mwaka sasa, lakini mtu hawezi kujua na pia napenda kuwa na uhusiano na mtu wa kawaida kabisa.
Over Ze Weekend: Hivi karibuni baba yako (Abdul Juma ‘Baba D’) alitoa kauli kali kuwa ikitokea ametangulia mbele ya haki usifike kwenye msiba wake akidai umemtukana, vipi kuhusu hilo unalizungumziaje?
Queen: Ni mambo ya kifamilia zaidi na pia yule ni baba yangu, ataendelea tu kuwa baba yangu daima.
Over Ze Weekend: Ukija kwenye upande wa uwifi hutabiriki kabisa uko upande gani maana kwa Zari ulikuwepo kwa Wema pia hadi kwa Penny, vipi kuhusu hilo?
Queen: Kwanza kabisa watu wajue nampenda Zari sana, lakini huko nyuma nilimpenda Wema kwa sababu alikuwa ndiye wifi kwa kipindi hicho, Penny ni rafiki yangu mpaka sasa bila kujali mambo ya uwifi.
Over Ze Weekend: Mbona hujamtaja wifi yako mmoja, namaanisha Hamisa Mobeto ambaye kawapa zawadi ya mtoto?
Queen: Hamisa ninachojua ni mama Abdul, lakini pamoja na hayo sina mazoea naye sana, tulikuwa tukionana juu kwa juu kwenye sherehe mbalimbali. Hata hivyo, Diamond hafuatilii kabisa uhusiano wangu na mimi kwa nini nimfuatilie?
Comments are closed.