Rais Joe Biden Aidhinisha Msaada wa dharura Kupambana na Moto – Live Updates
Rais Joe Biden wa Marekani ameidhinisha tangazo la msaada wa dharura wa serikali kuu kwa ajili ya kupambana na mioto ya msituni ya California, utakaofadhili utoaji wa fedha na rasilimali nyingine za kupambana na janga hilo.
Idara ya zima moto ya Kaunti ya Los Angeles imekumbana na mioto minne hatari kwa maisha, ambayo imesababisha vifo vya watu wawili na kuteketeza zaidi ya majengo 1,000, na kuwalazimisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao.
Mkuu wa idara zimamoto ya kaunti ya Los Angeles, Anthony Marrone amenukuliwa akisema idara yake ilijitayarisha kukabiliana na mioto miwili ya msituni na wala siyo minne, iliyosabaishwa na upepo mkali pamoja na uhaba wa unyevu nyevu hewani.
Amesema kuwa zaidi ya ekari 2,000 zimeungua, wakati moto ukiendelea kusambaa.