
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dk. Baghayo Abdallah Saqware kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).
Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Januari 4, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu inaeleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Dk Saqware alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA).
Taarifa hiyo imeongeza kuwa wengine walioteuliwa ni Charles Itembe anayekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Eneo Maalum la Mauzo ya Nje (EPZ) na Ernest Maduhu Mchanga ambaye anakuwa Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC).
Kabila ya uteuzi huo, Mchanga alikuwa Katibu Msaidizi, Fedha na Utawala, Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC) kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na kwamba uteuzi wa viongozi hao, umeanza Januari Mosi, 2021.
