Rais Samia Ampokea Rais wa Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi Ikulu jijini Dar (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amempokea Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi, katika hafla ya mapokezi rasmi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo, tarehe 02 Juni 2024.
Wakati wa mapokezi hayo, Rais Nyusi alikagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake pamoja na kupigiwa mizinga 21.
Kadhalika, MRais Nyusi alipata fursa ya kusaini kitabu cha wageni pamoja na kushiriki mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake, Rais Samia, yaliyofuatiwa na mazungumzo rasmi yaliyowashirikisha viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na Msumbiji.




