The House of Favourite Newspapers
gunners X

Ramaphosa Amkosoa Marekani: ‘Hujuma Dhidi ya Venezuela Inakiuka Mamlaka ya Nchi

0

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amepinga kikamilifu hujuma ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela ambayo amesema inadhoofisha mamlaka ya kujitawala na umoja wa kitaifa wa nchi hiyo mwanachama wa Umoja wa Mataifa.

Jana Jumanne Rais wa Afrika Kusini alitaka kuachiwa huru Rais Nicolas Maduro na mkewe na akikariri wito wa nchi hiyo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akilitaka kuchukua hatua madhubuti ili kutekeleza majukumu yake na kudumisha amani na usalama duniani.

Afrika Kusini juzi ililiaambia Baraza la Usalama kwamba mashambulizi ya upande mmoja ya Marekani dhidi ya Venezuela na hatua ya ovyo ya kumteka nyara Maduro na mkewe inakiuka uhuru na mamlaka ya kujitawala nchi.

Afrika Kusini imesema historia imeonyesha mara kwa mara kwamba “uvamizi wa kijeshi” dhidi ya nchi huru husababisha kukosekana utulivu na kuzidisha migogoro ikitoa mfano wa Libya, Iraqi na baadhi ya matukio barani Afrika. Imesema, uingiliaji kati wa nchi ajinabi umechochea ukosefu wa usalama na kudhoofisha taasisi za uongozi za kitaifa.

Rais Donald Trump wa Marekani Jumamosi iliyopita alitangaza kuwa oparesheni ya kijeshi ya nchi hiyo dhidi ya Venezuela imesababisha kutekwa nyara Maduro na mke wake, Cilia Flores na akaahidi kuwa iwapo italazimu ataidhinisha vikosi vya jeshi la nchi hiyo kuidhibiti Venezuela katika kipindi hiki.

MAJIBU ya KAKA wa LISSU TETESI za LISSU KUTOLEWA JELA kwa MARIDHIANO AKAKATAA – AFICHUA MAZITO….

Leave A Reply