The House of Favourite Newspapers

RASMI : CARDI B ATANGAZA KUACHANA NA OFFSET WA MIGOS (VIDEO)

Rapa wa kike Cardi B ametangaza kuachana na mzazi mwenzake, ‘Offset’  anayeliunda kundi la Migos siku ya jumanne Disemba 5.

 

Cardi B ametangaza taarifa hizo kupitia akaunti yake ya instagram kwa video inayomwonyesha akisema, “nimejaribu kuweka mambo sawa kwa muda kidogo na baba watoto wangu, na sisi ni marafiki wazuri  kwenye upande wa biashara na kama unavyojua nimekuwa muda mwingi namuongelea sana na tunapendana lakini kuna mambo ambayo hayajaweza kwenda sawa kwa muda mrefu, sio makosa ya mtu yoyote ila tumetoka nje ya upendo, hatupo pamoja tena.”Alisema Cardi B kwenye video.

 

Kumbuka pia Cardi B  na Offset walifunga ndoa ya siri mwaka jana na kuachana katika ndoa ni lazima wafwatilie maswala ya talaka. Kuhusiana na swala la talaka alisema, “ itachukua muda lakini nitaendelea kumpenda kwasababu ni baba wa motto wangu.

 

Cardi B na Offset wamefanikiwa kuapata motto mmoja wa kike anayejulikana kwa jina la Kulture Kiari Cephus  Julai mwaka huu.

 

Comments are closed.