Rayvanny kuimba nyimbo 25 Dar Live

ALICHOPANGA kufanya Rayvanny siku ya Idd Pili pale Dar Live kitalisimamisha jiji, kwa sababu atapiga nyimbo zake 25 bila kupumzika.

 

Rayvanny anakuja na usiku wa Vanny Day siku ya Idd Pili utakaofanyika Dar Live Mbagala ambako atapiga shoo kali mbele ya mashabiki wake wa Temeke na Mbagala kwa ujumla.

 

Ngoma kama Kwetu, Kishikwambi, Chuma Ulete mpaka kuwatetemesha mashabiki wake wote ambao watakijaza kiwanja cha Dar Live usiku huo kwa ngoma kali ya Tetema.

 

“Nitafanya shoo kali ambayo sijawahi kufanya popote tangu nimeanza kufanya muziki, nitaimba nyimbo 25 mfufulizo bila kupumzika na nitaangusha dansi ambalo sijawahi kudondosha popote,” alisema Rayvanny.

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam


Loading...

Toa comment