Rayvanny: Nitamfunika Harmonize Dar Live

MKALI wa Tetema kutoka katika lebo ya WCB, Raymond Shaban Mwakyusa ‘Rayvanny’ amesema shoo yake ya Vanny Day atakayoifanya siku ya Iddi Pili kwenye Ukumbi wa Dar Live, itakuwa ya kipekee na kuifunika shoo ya Harmonize.

 

Harmonize alipiga shoo kali mwaka jana kwenye Ukumbi wa Dar Live, ambapo sasa ni zamu ya Rayvanny ambaye amepanga kuweka historia ya kipekee kwenye usiku huo wa Vanny Day na kuifunika vibaya shoo ya Harmonize.

 

Akipiga stori na Championi Ijumaa, Rayvanny alisema anataka kuwapa kitu cha utofauti watu wa Temeke na kuvunja ile rekodi aliyoiweka Harmonize mwaka jana na kuweka historia ya kipekee itakayodumu kwa muda mrefu.

 

“Nataka nifanye shoo ya tofauti ambayo itaweka historia na kuvunja rekodi za wasanii wote ambao walishafanya shoo zao Dar Live, kuanzia Harmonize na wasanii wote waliowahi kupanda kwenye jukwaa lile, nitafanya mambo makubwa sana,” alimaliza Rayvanny.

 

Naye Meneja wa Burudani wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’, aliwataka wakazi wote wa Mbagala kuwa tayari kwani hawajawahi kukosea kufanya mambo makubwa kwenye ishu za kuandaa shoo.

Loading...

Toa comment