
MKUU wa Mkoa wa Dodoma nchini Tanzania, Antony Mtaka, ameuagiza uongozi wa ofisi ya mkurugenzi wa jiji na afisa elimu kuhakikisa wanawasambaza walimu wa sekondari katika shule zenye uhaba badala ya kuacha walimu kurundikana shule moja.
Mtaka amesema zipo shule za sekondari ndani ya Jiji la Dodoma ambazo zina walimu wengi na zipo shule za sekondari ambazo zipo pembezoni mwa jiji hilo zina walimu wachache.
“Kutoakana na hali hiyo, ofisi ya afisa elimu na ofisi ya mkurugenzi wa jiji waone namna ya kuweza kuwasambaza walimu waliokuwa wengi katika shule za mijini na kuwapeleka katika shule za pembezoni ambazo zina uhaba wa shule,” amesema.
Mtaka ametoa maelezo hayo leo Jumatano Desemba 22, 2022, wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondori kwa fedha za mkopo wa masharti nafuu unaotokana na mapambano dhidi ya Covid-19.