The House of Favourite Newspapers

REKODI ZA LIGI YA MABINGWA ULAYA

LIGI ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi imeanza jana, kila timu inataka ku­hakikisha inatwaa ubingwa huo ambao unashikiliwa na Real Ma­drid.

 

Hii ni michuano mikubwa sana ambayo imekuwa ikitikisa kwenye soka duniani kote, hakuna anaye­taka kutokea kwenye hatua hii kwa kuwa kila mmoja amekuwa akijizolea kiwango cha juu sana cha fedha aki­fanikiwa kuvuka hapa.

Zifuatazo ni rekodi za michuano hiyo hatua ya makundi, zipo nyingi sana lakini hizi ni baadhi tu.

Lionel Messi amecheza michezo 60 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufunga mabao 60.

Waliocheza mechi nyingi hatua ya makundi

Iker Casillas 89 ( Real Madrid, Porto)

Xavi Hernández 80 (Barcelona)

Cristiano Ronaldo 78 (Manches­ter United, Real Madrid).

Waliofunga mabao mengi

Lionel Messi, Cris­tiano Ronaldo (ma­bao 60)

Karim Benze­ma (mabao 40)

Aliyefunga mabao mengi kwenye mechi

Luiz Adriano mabao 4 (BATE Borisov 0-7 Shakhtar)

Aliyefunga mabao mengi msimu mmoja

Cristiano Ronaldo 12(Real Madrid, 2012/13)

Aliyefunga bao la mapema

Jonas (sekunde ya 10), (Valencia 3-1 Leverkusen, 01/11/11)

Bao la mapema la kujifunga

Iñigo Martínez, sekunde ya 2 (Manchester United 1-0 Real S o c i e d a d , 23/10/13)

Hat-trick ya mapema

B a f é t i m b i Gomis (dakika nane), (Dina­mo Zagreb 1-7 Lyon, 07/12/11)

Mchezaji kijana

Miaka 16, Celestine Babayaro (Steaua Bucureşti 1-1 Ander­lecht, 23/11/94)

Mchezaji mdogo kufunga bao

Miaka 17, Peter Ofori-Quaye (Rosenborg 5-1 Olympiacos, 01/10/97)

Mchezaji mzee zaidi

Miaka 43, Marco Ballotta (Real Madrid 3-1 Lazio, 11/12/07)

Mchezaji mzee kufunga

Francesco Tot­ti, miaka 38 (CSKA Moskva 1-1 Roma, 25/11/14).

Klabu iliyocheza hatua ya makundi mara nyingi

23 Barcelona, FC Porto, Real Madrid

22 Bayern, Man­chester United

Timu iliyofunga mabao mengi

Real Madrid mabao 321

Barcelona 293

Timu iliyopita kwenye makundi mara nyingi

Real Madrid 22

Timu iliyofunga mabao mengi msimu mmoja

Paris Saint-Germain mabao 25, (2017/18).

Comments are closed.