Ruby afunguka kuachana na mzazi mwenzake

KUACHWA au kuacha kusikie kwa wengine, usiombe yakukute! Hayo ni maneno ya mwanamuziki wa kike wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ ambaye juzikati zilisambaa tetesi kuwa ameachana na mzazi mwenzake, Kusah. Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Ruby alisema ameamini kuna watu wako macho kuona mwenzao anaachana na mpenzi wake ili wamcheke na kumuanika kwenye mitandao ya kijamii.

“Watu wanadhani kuachana ni rahisirahisi? Kuna watu wako macho kufurahia kile watakachosikia ili wakuanike kwenye mitandao, mimi na mzazi mwenzangu bado tupo sana, watatumbua macho hadi wachoke na kwa taarifa yao tunaongeza mtoto wa pili,” alisema Ruby


Loading...

Toa comment