The House of Favourite Newspapers
gunners X

Safari ya Mwisho ya Asia Mustapha: Aliyepambana na Maradhi ya Figo kwa Miaka 20 (Picha +Video)

0

Asia Mustapha, ambaye kwa muda wa takribani miaka 20 alikabiliana na changamoto za maradhi ya figo, ameaga dunia na kuhitimisha safari yake ya maisha kwa utulivu na heshima.

Mwili wa marehemu uliswaliwa katika Msikiti wa Maamur, Upanga, ukihudhuriwa na ndugu, jamaa na waumini waliokusanyika kumuombea dua. Baadaye, maziko yalifanyika katika Makaburi ya Kisutu, huku waliohudhuria wakimkumbuka kwa upendo, uvumilivu na imani yake iliyodumu hata nyakati za majaribu.

Tunamuombea Mwenyezi Mungu amsamehe madhambi yake, amlaze mahali pema Peponi, na awape faraja walioguswa na msiba huu.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Group, Abdallah Mrisho (kushoto mwenye miwani) akiwa katika maziko ya Asia katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam Disemba 24, 2025.
Mwili wa Asia ukiswaliwa katika Msikiti wa Maamur, Upanga.

Leave A Reply