Samatta Anavyoitamani Barcelona

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amefichua kuwa alitamani kuona timu yake inapangwa na klabu ya Barcelona au Real Madrid katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hivi karibuni timu ya Samatta, Genk ilipangwa kundi moja na Liverpool kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Samatta ambaye ni nahodha wa Taifa Stars na mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji ametoa kauli hiyo baada ya timu yake kupangwa kwenye Kundi H, wakiwa na Liverpool, Red Bull na Napoli.

Samatta alisema kuwa alitamani kuona wakipangwa na timu hizo za Hispania ili kuweza kutimiza ndoto yake lakini kwa kuwa wameangukia kwa Liverpool haoni shida yoyote.

“Kwanza nilitamani kuona tunapangwa na Barcelona au Real Madrid hiyo ndiyo ingekuwa furaha yangu kuona naweza kucheza dhidi ya timu hizo katika michuano hiyo lakini tumeangukia kwa Liverpool siyo mbaya japo uwanja wao umekuwa mgumu.

“Lakini niseme kwamba ukiangalia kwenye kundi letu sisi ndiyo wadogo peke yetu katika historia ya michuano hii, watu lazima waelewe kwa sababu Genk ina muda mrefu hajashiriki hivyo tumeingia kama wageni ambao tunahitaji kupata uzoefu mkubwa,” alisema Samatta


Loading...

Toa comment