The House of Favourite Newspapers

Samia Suluhu Amtembelea Tundu Lissu Nairobi Hospital (Video)

0
Samia Suluhu akimjulia hali Lissu.

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea na kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), na Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania (TLS), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi.

Samia amtembelea Lissu baada ya kumalizika kwa hafla ya kumwapisha Rais Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi.

Mhe. Samia Suluhu Hassan alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Lissu alikimbizwa katika hospitali hiyo baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana nyumbani kwake, Area D, Mjini Dodoma, Septemba 7 mwaka huu.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave A Reply