visa

Sanchi: Kwa siku natongozwa zaidi ya mara 100

BAADA kukaa kimya kwa muda mrefu ingawaje anakutana na vishawishi vingi, mwanamitindo mwenye umbo tatanishi, Jane Rimoy ‘Sanchi’ ameamua kufunguka kuwa anapata shida mitandaoni ambapo kwa siku anatongozwa zaidi ya mara 100.

 

Akizungumza na Za Motomoto ya Risasi, Sanchi alisema kuwa watu wasichokijua ana mtu wake lakini anakutana na usumbufu sana kwenye ukurasa wake wa Instagram (DM) kwa kupokea meseji za kutongozwa zaidi ya 100.

“ Unajua mtu akikuona kwenye mitandao vile anakuona anaweza kukupata kirahisi kumbe sivyo, kwanza mimi sitaki usumbufu jamani wajue na mimi ni mwanamke wa mwenyewe, wasichukulie maisha yangu ya mtandao ndiyo maisha halisi wajifunze hilo,” alisema Sanchi
Toa comment