The House of Favourite Newspapers

Sarah wa Harmonize Mikononi Mwa Sallam

0

MIONGONI mwa tuhuma nzito zilizotolewa na staa wa Bongo Fleva, Harmonize au Konde Boy Mjeshi siku ile ya Novemba 18, 2021 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, ni kitendo cha Lebo ya Wasafi kumtumia aliyekuwa mkewe, Sarah kumhujumu.

 

Sasa; katika kile kinachooneka kuwepo kwa ishara za ukweli wa jambo hilo, ni kitendo cha mkewe huyo ambaye walishaachana kuonekana akijiachia na mmoja wa mameneja wa Wasafi, Sallam SK.

 

Wikiendi iliyopita ya kusherehekea Mwaka Mpya 2022, Sarah na Sallam wanaonekana kwenye video iliyopostiwa na Sallam wakijiachia visiwani Zanzibar.

 

Taarifa zilizopatikana zilieleza kwamba, Sarah amekuwepo Zanzibar tangu wakati wa Sikukuu za Krismasi kabla ya Mwaka Mpya kuonekana mikononi mwa Sallam.

 

Katika madai yake, Harmonize alisema kwa sasa hawezi kuwa kwenye mapenzi na mwanamke wa Kibongo au anayefikika kirahisi kwani anaogopa yatatokea yale yaliyotokea kwa Sarah ambaye alikuwa akitumiwa na watu wa Wasafi kwa ajili ya kufuatilia nyenendo zake.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave A Reply