×

Serikali ya Mpito Yapendekeza Uchaguzi Usogezwe kwa Miaka 5

Serikali ya Mpito Nchini Mali, imependekeza mchakato wa kurejea katika utawala wa kidemokrasia kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2020 kusogezwa mbele kwa miaka mitano.

Awali, Serikali hiyo ilikubali kufanya Uchaguzi wa Rais na Bunge Februari 2022, miezi 18 baada ya Kanali Assimi Goita kuongoza Mapinduzi yaliyomtoa Rais Boubacar Ibrahim Keita Madarakani
ECOWAS imeiwekea vikwazo Mali kutokana na kuchelewesha Uchaguzi.

Leave a Comment