×

Serikali Yaandaa Tume ya Maridhiano Kuimarisha Umoja wa Kitaifa – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuwa Serikali imeanza maandalizi ya kuunda Tume ya Maridhiano ya Kitaifa, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha umoja na mshikamano wa Watanzania kuelekea mwaka 2026.

Akihutubia Taifa tarehe 31 Desemba 2025 kutoka Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar, katika salamu za kuukaribisha Mwaka Mpya 2026, Rais Samia alisema kuwa utulivu wa kisiasa, amani na usalama ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Rais Samia alieleza kuwa, pamoja na mafanikio yaliyopatikana mwaka 2025, Taifa pia lilipitia changamoto mbalimbali zilizoathiri wananchi, hasa katika kipindi cha mwezi Oktoba, hali iliyohitaji uvumilivu, umoja na uzalendo.

Aidha, alizishukuru taasisi za ulinzi na usalama pamoja na wananchi kwa kuendelea kudumisha amani na mshikamano, jambo lililoifanya Tanzania kuendelea kutambulika kama taifa imara na lenye uwezo wa kushughulikia changamoto zake kwa njia ya amani.

Akigusia Tume ya Maridhiano, Rais alisema Serikali itashirikisha wadau wote katika kubainisha muundo wa tume, aina ya wajumbe, majukumu na muda wa utekelezaji, kwa lengo la kuimarisha zaidi umoja wa kitaifa.

Leave a Comment