Serikali Yapongeza Uzalishaji wa Magari ya Umeme ya Ndani

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Patrobas Katambi, akiwa ameambatana na Mkurugenzi Msaidizi wa Sera, Utafiti na Ubunifu, Audax Bahweitima, akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara, ametembelea karakana ya kuzalisha magari madogo yanayotumia nishati ya umeme ya KAYPEE MOTORS wakati wa ziara yake katika TIRDO, tarehe 22 Desemba 2025, jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, Katambi amejionea hatua za uzalishaji na ubunifu wa teknolojia ya ndani, akisisitiza dhamira ya Serikali kuendelea kuhimiza viwanda vya ndani, nishati safi, na ubunifu unaochochea uchumi wa kijani pamoja na ajira kwa vijana.


