The House of Favourite Newspapers

SEVILLA WAIPA ‘BIG UP’ SIMBA KWA KUTWAA UBINGWA

KIKOSI cha klabu ya Sevilla FC cha nchini Hispania ambacho kimewasili nchini usiku wa kuamkia leo na kupokelewa kwa shangwe kubwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kupitia kikundi cha ngoma kilichopo chini ya msanii Mrisho Mpoto, wameipongeza Simba kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar, Rais wa Sevilla FC, José Castro, amesema: Niwapongeze sana Simba ya Tanzania kwa kuchukua ubingwa wa ligi Kuu.  tumekuja kucheza na timu bora, ni heshima sana kuja Tanzania na bila shaka tutakuwa ni timu ya kwanza ya Laliga kuja Tanzania.”

Simba jana ilicheza na Singida United, mkoani humo,  na kuifunga mabao 2-0, jambo lililoifanya Sevilla,  kupitia ukurasa wao wa Twitter,  kuipongeza timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi jijini Dar.

 

Kwa upande wao TFF wamesema; “Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ina ushirikiano wa miaka mitatu na La Liga hivyo ujio wa Sevilla kuja kucheza na Simba ni ishara kwamba ushirikiano wetu ni mkubwa, SportPesa imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika kusaidia maendeleo ya michezo,” amesema Rais wa TFF, Wallace Karia.

 

 

Sevilla wamekutana na mafundi makinda wa timu ya BOM BOM katika kliniki waliyoendesha leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Comments are closed.