Shetta Achaguliwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam

Diwani wa Kata ya Mchikichini, Nurdin Bilal maarufu Shetta, amechaguliwa kuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam. Uchaguzi huo ulifanyika kwa kishindo, ambapo Shetta alipata kura 48 kati ya kura 51 zilizopigwa.
Uchaguzi huu unamweka Shetta katika nafasi muhimu ya kuongoza na kusimamia masuala ya maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam, huku akitarajiwa kuimarisha huduma kwa wakazi na kusimamia miradi ya maendeleo.

