Shigongo Katika Mkutano Wa IPU Aelezea Umuhimu Wa Afrika Kutumia Maliasili – Video

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo ameshiriki Mkutano wa Mabunge ya Dunia (Interparliamentary Union) unaofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York Nchini Marekani.
Mkutano huo unajadili jinsi dunia, ikiwemo Tanzania, itakavyotimiza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kama kuondoa umasikini, ujinga, na vifo vya kinamama.
Eric Shigongo ambaye pia ni mjasiriamali, mfanyabiashara na mtunzi wa vitabu, ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe huu baada ya mkutano huo:
Nimepata fursa ya kushiriki Mkutano wa Mabunge ya Dunia (Interparliamentary Union) unaofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York.
Katika mkutano huu, tunajadili namna ambavyo dunia, ikiwemo Tanzania, inaweza kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), yakiwemo kuondoa umasikini, ujinga, na kupunguza vifo vya kina mama.
Ni heshima kubwa kuwa sehemu ya majadiliano haya yenye lengo la kujenga dunia yenye usawa na maendeleo kwa wote.