The House of Favourite Newspapers

SHOGA: MTINDI HAUTENGENEZI CHAI

0

SHOGA: MTINDI

HEEEE heeeeiyyaaaaa shoga yangu wa ukweee upo? U hali gani Jumanne ya leo! Kama nakuona vile ulivyotoa mijicho kama mwari aliyevalishwa, kapakwa ina hadi kwenye unyayo, karembeshwa wanja huooo kisha mwisho wa siku akaambiwa bwana harusi amekataa kumuoa? Haloooo nicheke miye mbavu zangu ziishi!

Shoga leo sitaki kuongea sana, nimechoka kabisaa na malalamiko ya baadhi yenu ‘ohh MC Sophy anaongea sana sijui anafundisha kiduchu mara ohh mwisho wa siku anatuacha kwenye mataa tukitamani mada iendelee’ aliyekuacha kwenye mataa nani sasa mi au wewe usiyefundishika?

Uliyezamia jiji kwa baiskeli na fungo la rambo lililojaa nguo! Kama ulikuwa hujui sasa leo nimekuja kivingineee! Nyie mnaolazimisha mtindi utengeneze chai mkiamini itatoka chai ya maziwa! Siongei na wewe mwanamke mwenzangu leo nipo na hawa kina baba!

Nikisema kina baba naomba mnisikie na kunisoma kwa makini msije kusema MC Sophy kila siku anawaambia wanawake tu! Kuna wakina baba ukisikia matatzio yao lazima uwaonee huruma ati! Yeye kufunga magoli ya mapema imekuwa tatizo, tena sekunde chache amejilaza nje ya uwanja na anavua jezi kabisa anahema kama mkulima wa vitunguu akimaliza kufunga gunia lake.

Hii imekuwa ikiwaumiza sana kina mama sawa na kipa aliyefanya mazoezi ya kuzuia mashuti makali lakini baada ya yangu wa ukweee upo? U hali gani Jumanne ya
mpira kuanza mshambuliaji akupigie shuti kama mate ya mvuta bangi, inaudhi kwa kweli! Kibaya zaidi anatoka nje ya uwanja na kukuacha ukiteseka na kukimbilia kujikanda na maji ya moto kila siku mwisho kutaota sugu na kuua virutubisho na kuondoa ladha.

Japo si mtaalamu sana wa mambo hayo lakini kuna kitu nilikutana nacho ambacho kilinipa somo na kuona kuna umuhimu wa kuwaeleza akina baba wengine nao wajaribu kutumia njia hii.

Kuna msomaji alishawahi kuniambia kuwa alikutana na mwanaume mmoja ambaye ukimuangalia utajua hana kasoro yoyote basi kama kawaida akaingia naye kwenye shamba lake la minazi. Mwanamke akaanza kuukwea huku akitatalika kama bisi za kula kwenye sinema, kijana wa watu Mungu alimjalia sura, nguvu na uwezo wa kuuyumbisha mnazi wake kimadaha.

Lakini kabla hajafi kia madafu ili anywe maji yake, alimuwahi na kulitupa dafu chini likamwagika akalazimisha tena na kufanikiwa kurudi alipotoka. Alimueleza kuwa kutokana na ugumu wa shughuli zake zimemfanya apungue uwezo wa kuangusha madafu mengi, kama dafu la kwanza angelipasulia ndani asingeweza kumfurahisha.

Alisema mtindi hauwezi kutengeneza chai, ukilazimisha kuchukua maziwa ya mtindi ukayachemsha lazima yapande juu na kujenga tope sa hayo majani ya chai utaweka wapi? Utakunywaje hiyo chai kwa mfano? Kwa leo niishie hapa najua umenielewa somo langu, tukutane tena wiki ijayo! Namba yangu hiyo hapo juu, tuma meseji tu kwa maoni na ushauri.

NA: MC Sophia (0713 761 135)| UWAZI

Leave A Reply