Shoo ya Miss Tanzania ni leo, kiingilio Sh 75,000

 

KINYANG’ANYIRO cha kumsaka mrembo atakayerithi taji la Miss Tanzania kinatarajiwa kufanyika leo Ijumaa kwenye Ukumbi wa LAPF uliopo Jengo la Millenium Tower, Kijitonyama Dar huku kiingilio kikiwa ni Sh 75,000.

 

Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi amesema warembo 20 kutoka kanda mbalimbali za kimikoa watashiriki.

Basilla alisema mshindi atakayefanikiwa kurithi taji hilo kutoka kwa mrembo aliyepita Queen Elizabeth Mkune ndiye atakayekuwa mwakilishi wa mashindano dunia ambayo yanatarajiwa kufanyika Uingereza, Desemba 14, mwaka huu.

 

Amewaomba mashabiki wa urembo kufika mapema ukumbini hapo ili kujionea mashindano hayo yakiwa na muonekano tofauti na siku za nyuma na kuongeza kuwa sambamba na mpambano huo pia kutakuwa na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya akiwemo Barnabas Elius


Loading...

Toa comment