The House of Favourite Newspapers

Simba Kukipiga Dhidi ya Power Dynamos Simba Day – Video

0

 

 

Meneja wa Habari wa klabu hiyo Ahmed Ally

Klabu ya Simba imethibitisha kuwa kwenye kilele cha Wiki ya Simba Day, Wekundu hao wa Msimbazi watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Ligi Kuu Zambia 2022/23, klabu ya Power Dynamos

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Meneja wa Habari wa klabu hiyo Ahmed Ally amebainisha kuwa viingilio Vingilio vya Simba Day vitakuwa kama ifuatavyo:-
Platinum Tsh. 200,000,
VIP A – Tsh. 40,000,
VIP B Tsh. 30,000,
VIP C Tsh. 20000,
Machungwa – Tsh. 10,000 na
Mzunguko Tsh. 5,000.

“Kwa upande wa vingilio, sisi kama klabu tunahitaji fedha lakini kwenye tamasha tunahitaji zaidi mashabiki, Wanasimba waje zaidi ndio maana tunawatafuta wadhamini kama CRDB ili walete fedha. Tunajali zaidi maslahi ya Wanasimba.” amesema

“Kispika kinarudi mtaani kuwaita Wanasimba kwenye Simba Day. Tunaenda kuwaonyesha kwamba Uwanja wa Mkapa ni mdogo sana kwa Simba kuujaza.”

“Waliopandisha kibegi kwenye Mlima Kilimanajaro, watu wote tisa tutawaalika kwenye Simba Day na watapata nafasi ya kutambuliwa na mashabiki kwenye siku ya tamasha letu.”

“Kikosi kitarejea kutoka Uturuki tarehe 1 ya mwezi Agosti.”

“Unyama Mwingi ni usajili mzuri, tamasha kubwa, kutimiza malengo ambayo tumejiwekea ya kuchukua mataji yote ya ndani na kufanya vizuri kimataifa.”
“Wiki ya Simba itazinduliwa tarehe 29, Julai – tarehe 6 ya mwezi Agosti. Matukio ni kama kuchangia damu, shughuliza kijamii kufanya usafi kwenye hospitali, masoko lakini pia tutakuwa na siku maalumu ya kutembelea mashujaa wa Simba.”
“Uzinduzi wa Simba Week tutafanya eneo la Buza Kanisani. Itakuwa tarehe 1, Agosti na tutaanza saa 4 asubuhi. Tunataka kufanya uzinduzi mkubwa na wa kihistoria. Wanasimba mjiandae.”
“Simba Day tutacheza na bingwa kutoka Zambia, timu ya Power Dynamos. Huyu ndio tutacheza nae kwenye kilele cha Simba Week.”
“Kwa upande wa wasanii watoto wa nyumbani, Tunda Man, Meja Kunta na Whozu watakuwepo. Siku zinapokwenda tutaendelea kutangaza wasanii wengine ambao watakuwepo.”- amesema Ahmed Ally.

Leave A Reply