The House of Favourite Newspapers

Simba Queens Yaichakaza Vibaya Yanga Princess

0

SIMBA Queens imeendeleza rekodi ya ubabe mbele ya Yanga Princess kwa kuendeleza vipigo kwenye msimu wao wa nne mfululizo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa leo Uwanja wa Mkapa Dar es salaam.

 

Simba Queens imeweka rekodi ya kushinda mechi sita kati ya saba ilizowahi kukutana na Yanga kwenye ligi.

 

Takwimu zinaonyesha kwamba msimu wa 2018/19, Simba Queens ilishinda mabao 7-0 kwenye mchezo wa
mzunguko wa kwanza kisha mabao 5-1 kwenye mzunguko wapili na msimu wa 2019/20 waliendeleza ubabe kwa
kushinda mabao 3-1 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza kabla ya mzunguko wapili kushinda mabao 5-1.

 

Msimu uliopita mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga iliambulia sare ya bila kufungana kule Mo Bunju Arena kabla ya kufungwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa mzunguko wapili.

 

Ushindi huo umeifanya Simba kurudi kileleni kwenye msimamo wa ligi na kuishusha Fountain Gate ambayo ilikuwa inaongoza kwa alama tisa wakati Simba baada ya kushinda imekusanya alama 11.

Mabao ya Simba yalifungwa na Oppah Clement aliyefunga mawili pamoja na Asha Djafar ambaye pia alifunga mawili huku bao pekee Yanga likufungwa na Aisha Masaka kwa mkwaju wa penalti.

 

Vilevile Simba inakuwa imeshinda mechi ya nne mfululizo tangu ianze ligi kwa msimu huu jambo ambalo linaiweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea taji lao walilochukua msimu uliopita.

FT: Yanga Princess 1-4 Simba Queens

Simba

⚽️Asha Djaral (7′, 81′)
⚽️Opa Clement (54′, 70′)

Yanga

⚽️Aisha Masaka 77′ (p).

Leave A Reply