The House of Favourite Newspapers

Simba Yabadili Gia Kwenye Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula

UONGOZI wa Simba, umeweka wazi kuwa, utarejea ukiwa imara zaidi na mwendo mwingine kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutinga hatua ya makundi.

Ikumbukwe kwamba, Simba ilifanikiwa mpango kazi kutinga hatua ya makundi kwa faida ya bao la ugenini dhidi ya Power Dynamos.

Kwenye mchezo wa kwanza ugenini, ubao ulisoma Power Dynamos 2-2 Simba, kisha marudiano nyumbani ni Simba 1-1 Power Dynamos. Matokeo ya jumla Simba 3-3 Power Dynamos.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula, amesema kutinga hatua ya makundi yalikuwa ni malengo yao, kinachofuata ni maandalizi kwenye mechi zijazo.

“Kupata nafasi ya kufuzu hatua ya makundi sio jambo dogo, unaona tulicheza na timu ambayo ilikuwa na upinzani mkubwa. Power Dynamos sio ya kuibeza, ilishawahi kutwaa ubingwa wa Shirikisho Afrika.

“Kuelekea kwenye hatua ya makundi, kuna maboresho ambayo yatafanyika kwenye maeneo tofautitofauti ili kuwa na mwendelezo mzuri katika kupata matokeo mazuri,” alisema Kajula.

STORI NA LUNYAMADZO MYUKA

MAMA WARDA AKUTANA USO KWA USO NA MWALIMU WEMA, VILIO VIPO PALEPALE | MAPITO