The House of Favourite Newspapers

SIMBA YAIHARIBU VIBAYA COASTAL, BAO 8-1 ZAIPELEKA KILELENI

KLABU ya Simba imetinga kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuipiga kipigo hevi cha bao 8-1, timu ya Coastal Union ya Tanga leo Jumatano, Mei 8, 2019.

Mabao ya Simba Sc

Emmanuel Okwi (dakika ya 11′, 20′ na 47′)
Meddie Kagere  (dakika ya 69′, 75′ na 83′)
Hassan Dilunga (dakika ya 81′)
Clatous Chama (90+2)


Bao pekee la Coastal Union limefungwa na ⚽Raizan Hafidh (dakika ya 35). Raizin Hafidh ndio alifunga bao pekee wakati Simba ikishinda 2-1 dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani. Leo amefunga tena dhidi ya Simba.

 

Okwi amefikisha magoli 13 kwenye ligi msimu huu, anawakimbiza Heritier Makambo (16), Salim Aiyee (16) na Meddie Kagere (17).

Okwi na Kagere wameondoka na mipira kwa kutupia Hattrick.

Emmanuel Okwi amefunga magoli 3 dhidi ya Coastal Union (hat-trick) na kuikisha magoli 14 kwenye ligi akiwakimbiza Salim Aiyee (16), Heritier Makambo (16). Meddie Kagere amefikisha magoli 19 Ligi Kuu, anaendelea kuongoza chat ya wafungaji bora msimu huu.

 

Rekodi ya Simba msimu huu.

🏟Mechi 31
🧾Pointi 81
✔Ushindi 26
🤝🏼Sare 3
❌Vipigo 2
⚽Magoli ya kufunga 69
🥅Magoli ya kufungwa 13.

Comments are closed.