Simba Yajibu Mapigo Usajili wa Yanga

KOCHA wa Simba,Patrick Aussems amesisitiza kwamba usajili utakaofanyika wa wachezaji wa kigeni utakuwa na kishindo cha aina yake na hakuna timu ya Tanzania itakayoweza kuwafi kia ikiwemo Yanga.

 

Yanga tayari imeshasajili mashine saba za kigeni huku wakisisitiza kwamba wanafanya usajili kabambe. Mbelgiji huyu ambaye sasa yupo likizo kwao amesema atasajili wapya watano wa maana na wenye vigezo vya kipekee na uwezo wao lazima uwe mithili ya Meddie Kagere na Clatous Chama au kuzidi.

 

Spoti Xtra linafahamu wa kwanza kabisa ni Francis Kahata wa Gormahia ya Kenya akifuatiwa na Juma Balinya wa Polisi ya Uganda ambao dili zao ziko freshi. Alisema kwamba mastaa hao wapya wengi wao lazima wawe walishacheza michuano ya kimataifa kufi kia levo ya robo fainali na hataki mtu wa kubahatisha.

 

Kati ya masharti yaliyopo kwenye mkataba mpya wa Aussems ni kuhakikisha anatetea ubingwa wa Bara, anabeba SportPesa Super Cup, Kombe la Mapinduzi na kurejesha kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

 

“Mpango wangu ni kusajili wachezaji wa nje ambao watakuwa na uzoefu zaidi kimataifa hasa kwenye hii michuano ya Afrika ya Ligi ya Mabingwa ambao wamefi ka hatua kuanzia robo fainali kwenda mbele hao wanakuwa na uzoefu wa kutosha.

 

“Ukiangalia katika kikosi changu unakuta wachezaji ambao wana sifa kama hizo ni Kagere na Chama, hivyo ni lazima niangalie hilo ili kuwa na kikosi imara,” alisema Aussems ambaye mshahara wake ni Sh.Mil 27 kwa mwezi na kuongeza.

 

“Wachezaji kimataifa watano wataondoka ndani ya kikosi na nitajaza nafasi zao, nahitaji kusajili nafasi zote kuanzia mbele lakini si nafasi ya kipa.

 

Wachezaji wangu niliwaeleza kila kitu.” Spoti Xtra linajua kwamba Wachezaji wa kigeni wanaopigwa chini Simba ni Juuko Murshid, Zana Coulibaly, Asante Kwasi, Nicholas Gyan na Haruna Niyonzima. Muwezeshaji wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amekubali kumnunulia kocha huyo mchezaji yoyote yule hata Ulaya.

 

Mo alisisitiza wiki iliyopita kwamba anataka kusajili wachezaji wenye kiwango kikubwa na atashindana na klabu kubwa za Afrika ikiwemo TP Mazembe.

Toa comment