Simba Yatambulisha Mtendaji Mpya, Magori Aachia Ngazi

KLABU  ya Simba  leo imemtangaza Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mazingiza, ambaye anachukua nafasi ya Crescentius Magori aliyemaliza muda wake. Mazingiza amewahi kuwa mtendaji mkuu (CEO) wa vilabu ya Platinum Stars na Orlando Pirates vya South Africa.

 

Ametambulishwa leo Jumamosi, Septemba 7, 2019,  jijini Dar es Salaam ambapo Magori amesema Mazingisa ataanza kazi rasmi Jumatatu wiki ijayo wakati yeye sasa anastaafu.

“Kuanzia wiki ijayo nitakuwa CEO mstaafu. Nawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipa.

Nawashukuru sana wana-Simba. Kwa tuliokwazana niwaombe radhi ilikuwa sababu ya kazi yangu,” amesema Magori.


Loading...

Toa comment