The House of Favourite Newspapers

SIMBA YAZIDI KUKWEA KILELENI, YAICHAPA MTIBWA 2-1, KAGERE ATUPIA

 Kikosi cha Simba kimeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara leo.

Ushindi huo umepatika kupitia mabao ya Meddie Kagere dakika ya 17 kipindi cha kwanza na Miraji Athumani akifunga dakika ya 68 kipindi cha pili.

Kabla ya Miraji kuongeza bao la pili, kipindi cha kwanza Riffat Khamis aliisawazishia Mtibwa dakika ya 20 ikiwa ni dakika tatu pekee Kagere acheke na nyavu na matokeo kuwa 1-1.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Simba walikuwa na mabao mawili huku Mtibwa wakiwa na moja.

Ushindi huo umewafanya Simba kufikisha jumla ya alama sita wakiwa kileleni mwa ligi.

Wakati huo, KMC nao waliokuwa ugenini Mkwakwani Tanga kucheza dhidi ya Coastal union wamelala kwa mabao 2-0 kutoka kwa Wagosi hao wa Kaya.

Comments are closed.