The House of Favourite Newspapers

Simbomana, Bigirimana wafichua kilichowaleta Yanga

UONGOZI wa Yanga tayari umeshakamilisha usajili wa nyota wa kigeni kutoka Rwanda, Patrick Sibomana ‘Papy’ na Issa Bigirimana ‘Walcott’ wameweka wazi sababu kubwa ya kujiunga na timu hiyo. Sibomana ambaye alikuwa winga wa Mukura Victory ya Rwanda na mshambualiji wa APR raia wa Rwanda mwenye asili ya Burundi, Bigirimana wote wamesaini mikataba ya miaka miwili kabla ya kukwea pipa kurejea Rwanda.

 

Nyota hao wa kimataifa ni miongoni mwa wachezaji wapya wa Yanga watakaoitumikia timu hiyo katika msimu ujao. Wakizungumza na

Championi Ijumaa wakiwa nchini Rwanda kwa nyakati tofauti, nyota hao walisema malengo yao ni kuona Yanga inafika mbali ikiwemo kuchukua ubingwa wa ligi kuu. Sibomana alisema:” Ni kweli nimesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kucheza Yanga msimu ujao.

 

“Nataka kufika mbali na hii ni timu kubwa naamini nitaweza kufikia ninapotaka pale ligi itakapokuwa imeanza maana kitu kikubwa ni ubingwa ili tushiriki michuano ya kimataifa.”

 

 

Kwa upande wa Bigirimana alisema: “Nimekamilisha usajili nimerudi nyumbani kujipanga kwa ajili ya msimu mpya nikiwa Tanzania, nimejipanga kupambania namba pamoja na kuisaidia timu yangu kufikia malengo yake, kikubwa ushirikiano ndiyo itakuwa silaha yetu.”

Comments are closed.