Siri Yafichuka Bale Kuigomea Real

SIRI imefichuka ya kisa cha fowadi wa Real Madrid, Gareth Bale kugoma kuondoka klabu hiyo licha ya kutotakiwa na kocha Zinedine Zidane. Bale ameapa kuwa atarejea katika kikosi hicho mwezi Julai wakati watakapoanza kambi ya mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao.

 

 

Kufuatia msimamo huo, Bale aligoma kuaga wenzake na hata mashabiki kwenye mechi ya mwisho ya La Liga dhidi ya Real Betis, wikiendi iliyopita. Zidane amemweleza wazi staa huyo mwenye umri wa miaka 29 kuwa hayumo katika mipango yake.

 

Hata hivyo, watu walio karibu na Zidane wanadai kuwa Bale amegoma kuondoka kwa sababu ya mshahara mnono anaolipwa na Real Madrid. Bale analipwa kitita cha pauni milioni 15 kwa mwaka (Sh. bilioni 43), ambapo sasa hataki kuondoka na kuachia mshahara huo.

 

Staa huyo ameamua hawezi kuondoka na kuachia mshahara huo mkubwa wakati amebakiza miaka mitatu katika mkataba wake na klabu hiyo. Tangu Zidane arejee katika timu hiyo, uhusiano kati ya watu hao wawili umekuwa sio mzuri.

MADRID, HISPANIA


Loading...

Toa comment