Siwema amshushia sifa Nay wa Mitego

 MREMBO ambaye ni mzazi mwenziye na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ Siwema Edson amesema hawezi kuwa mchoyo wa kutoa pongezi kwa mzazi mwenziye huyo kwa jinsi anavyomlea mtoto wao, Curtis kwa sababu ni baba bora. Akizungumza na Za Motomoto ya Risasi, Siwema alisema kuwa ,hata kama wana tofauti lakini kwa upande huo anampa hongera kwa sababu hata hivyo alimuacha mtoto akiwa mdogo kutokana na matatizo ya hapa na pale lakini Mungu ni mwema alijitahidi kumlea kwa mapenzi makubwa.

“Unajua siwezi kumsema Nay kwa mabaya tu maana mambo yalishapita kitambo sana, il a ukweli najivunia ni baba bora kwa mtoto wetu na hata kama hatupo pamoja lakini mtoto ahisi tofauti kabisa kutokana na mapenzi makubwa anayopata kutoka kwa baba,” alisema Nay ambaye anaendelea na maisha yake jijini Mwanza.


Loading...

Toa comment