The House of Favourite Newspapers

Straika Aaga Kwao DR Congo, Rasmi Kutua Simba

0
Eric Kabwe

RASMI mshambuliaji wa AS Vita ya DR Congo, Eric Kabwe ameaga ndani ya timu hiyo huku akiweka wazi hatakuwepo kwani amefikia sehemu nzuri ya kujiunga na Simba chini ya Kocha Mbrazil, Robertinho Oliviera.

Kabwe ambaye anamudu kucheza nafasi zote za mbele kwa maana ya winga wa kushoto na kulia na mshambuliaji wa kati, ni moja kati ya usajili ambao tayari umeshakamilika ndani ya Simba.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kabwe amethibitisha kuondoka na AS Vita mara baada ya msimu kumalizika huku pia akiweka wazi safari yake ya kutua Simba imekamilika kwa asilimia 90.

“Sitakuwepo ndani ya AS Vita msimu ujao, sitakuwa sehemu ya kikosi na nawashukuru wote ambao nimeshirikiana nao kwa kiasi kikubwa ndani ya timu hiyo kwa kuwa wana mchango mkubwa kwangu mpaka sasa kuwa nilipo.

“Kuhusiana na Simba ni kweli kila kitu kipo sawa na naweza kusema kwa asilimia 90 usajili ulishakamilika na natarajia kujiunga na timu hiyo msimu wao utakapoisha, matarajio yangu ni hayo na natamani kuona yanatimia kutokana na ukubwa wa Simba,” alisema mchezaji huyo.

Stori na Marco Mzumbe

Leave A Reply