The House of Favourite Newspapers

Straika Kiboko wa Yanga Aandaliwa Mkataba Simba

0
Mshambuliaji wa Vipers, Milton Karisa.

IMEELEZWA kwamba, mshambuliaji wa Vipers, Milton Karisa, atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Simba katika kipindi kijacho cha dirisha kubwa msimu ujao wa 2023/24.

Ujio wa mshambuliaji huyo unakuja kuiboresha safu hiyo ya ushambuliaji ya Simba ambayo msimu huu inaongozwa na Jean Baleke, John Bocco na Moses Phiri.

Karisa aliisumbua safu ya ulinzi ya Yanga wakati timu yake ya Vipers ilipocheza mchezo wa kirafiki katika Wiki ya Mwananchi mwanzoni mwa msimu huu.

Mbali na Karisa, wapo baadhi ya washambuliaji wanaotajwa kusajiliwa na Simba kuelekea usajili wa msimu ujao, kati ya hao ni Victorien Adebayor raia wa Niger.

Mmoja wa mabosi wa Simba, ameliambia Spoti Xtra kuwa, mshambuliaji huyo anasajiliwa na Simba kutokana na mapendekezo ya Kocha Mkuu, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ aliyekuwa anamfundisha akiwa Vipers.

Bosi huyo alisema, Karisa anakuja Simba kuchukua nafasi ya Mghana, Augustine Okrah ambaye tayari ameomba avunjiwe mkataba ili aondoke.

Aliongeza kuwa, mazungumzo yamefikia pazuri na huenda mshambuliaji huyo akasaini mkataba mara baada ya Ligi Kuu Bara msimu huu kumalizika.

“Karisa mwenyewe ameonesha nia ya kujiunga na Simba katika msimu ujao baada ya kufikia muafaka mzuri na uongozi wakati wa majadiliano.

“Usajili wake umekuwa mwepesi kutokana na uwepo wa Robertinho ambaye aliwahi kumfundisha kipindi akiwa Vipers kabla ya kuja Simba.

“Ushawishi mkubwa aliutoa Robertinho kwa Karisa ambaye huenda akawa mchezaji wa kwanza kusajiliwa Simba,” alisema bosi huyo.

Akizungumzia hilo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema kuwa: “Tumepanga kukiboresha kikosi chetu kuelekea msimu ujao, hivyo usajili wetu unatarajiwa kuwa bora kwa kuwasajili wachezaji wenye sifa wataorejesha heshima ya Simba katika michuano ya kimataifa na ile ya ndani.”

STORI NA WILBERT MOLANDI

UBAYA, SHIJA KUPANDA ULINGONI JUNI 29, JAPHET KASEBA, PENDO NJAU WAFUNGUKA MAZITO…

Leave A Reply